Habari Mseto

Wanaswa wakisafirisha magunia 230 ya makaa

June 7th, 2020 1 min read

NA GERALD BWISA

Maafisa wa Huduma za Misitu kutoka kitengo cha upelelezi walikamata malori mawili yaliyokuwa yakisafirisha magunia 230 ya makaa kutoka kaunti ya Trans Nzoia.

Afisa anayesiamia huduma za misitu Trans Nzoia George Simbe aliiyeongoza oparesheni hiyo alisema kwamba washukiwa hao walikamatwa.

Dereva wa lori hilo Geoffrey Ngatia, Richard Lakawa na Bonface Wakasala walikamatwa kwa kusafirisha magunia 160 kinyume na sheria katika barabara kuu ya Kitale-Webuye.

Kwa kisa kingine Dorice Omondi an Geoffrey Chege walikamatwa pia wakisafirisha magunia 70 ya makaa katika barabara ya Kapenguria-Kitale.

Washukiwa hao watatu walifungiwa kwenye kituo cha polisi cha Kitale na baadaye kuachiliwa kwa faini ya Sh10,000 kila mmoja. Watajitokeza tena kortini Julai 3, 2020.

Waliokamatwa kwenye barabara kuu ya Kapenguria-Kitale watajitokeza tena kortini Julai 7, 2020.