Wanaume wamo hatarini zaidi kuugua figo – Wataalamu

Wanaume wamo hatarini zaidi kuugua figo – Wataalamu

NA CECIL ODONGO

WANAUME ndio wapo katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa wa figo, wataalamu wamebaini.

Utafati uliofanywa na wataalamu wa Chuo Kikuu cha Catholic Sacred Heart jijini Milan unaonyesha kuwa ugonjwa huo huingia na kusambaa kwa wanaume haraka ikilinganishwa na wanawake.

Kulingana na watafiti hao, wanaume hupata ugonjwa wa figo kutokana na kuwa wengi wao wana historia ya kupata magonjwa ya shinikizo la damu, sukari na mtindo wao wa maisha.

Pia, matumizi ya dawa za kupambana na shinikizo la damu hasa miongoni mwa wanaume kunawaweka katika hatari ya kupata ugonjwa huo hatari.

Aidha, utafiti huo ulibainisha kuwa wanaume wana kiwango cha juu cha madini aina ya calcium mwilini na pia mkojo wenye asidi nyingi. Madini na asidi hizo ni kati ya yanayosababisha ugonjwa wa figo.

Pia wanaume hupenda kula vyakula vyenye protini na chumvi nyingi na mambo haya mawili huchangia sana kupata ugonjwa wa figo. Vilevile wanaume hunywa maji kwa uchache sana ikilinganishwa na wanawake ilhali kunywa maji mengi kunasaidia kupunguza uwezekano wa kupata figo.

Kwa wanawake, hatari ya kupata ugonjwa wa figo upo chini isipokuwa kwa wale ambao wamenenepa zaidi na pia wasiosafisha vyema uke wao ambao mkojo hupitia.

“Kwa wanaume pia ugonjwa wa figo unaweza kutambuliwa mapema kuliko wanawake ila huwa hawafiki katika vituo vya kimatibabu kufanyiwa uchunguzi. Hata hivyo, figo kwa wanawake huwa ni vigumu sana kutibu ikilinganishwa na kwa wanaume kwa sababu ya maambukizi kwenye njia ya mkojo,” ukasema utafiti huo.

  • Tags

You can share this post!

BORESHA AFYA: Vyakula kutuliza uchungu wa hedhi

Mbona mwasho mkali kwenye chuchu zangu?

T L