Wanawake Garissa walalamika kunyanyaswa kisiasa kupitia demokrasia ya maelewano

Wanawake Garissa walalamika kunyanyaswa kisiasa kupitia demokrasia ya maelewano

NA KENYA NEWS AGENCY

BAADHI ya wagombeaji wa kike katika kaunti ya Garissa wamelalamikia mfumo wa demokrasia ya maelewano unaotumika eneo hilo wakisema unatumiwa kuwanyima nafasi za kuwania viti.

Wanawake hao walisema mfumo huo unawapendelea wapinzani wao wa kiume, jambo ambalo walisema ni kinyume cha misingi ya kidemokrasia.

Wakiongea katika mkutano ulioandaliwa na muungano wa Wabunge wa Kike (KEWOPA) wanasiasa hao pia walitaja ukosefu wa fedha, mila potovu kama vikwazo vinavyowazuia kupata viti vya uongozi.

Mmoja wao, Jamila Farah, ambaye alikuwa akipanga kuwania kiti cha udiwani wa wadi ya Jarajara katika eneo bunge la Balambala alilalamika kuwa alishauri kujiondoa ili kumpisha mgombeaji wa kiume.

“Badala yake nilishauriwa kuwania kiti cha Mbunge Mwakilishi wa Kike, inayochukuliwa kama ndio ya wanawake,” akaeleza.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

BAHARI YA MAPENZI: Kuboresha uhusiano baada ya ugomvi

Ukora wa bunge la 12 na kamati zake

T L