WANDERI KAMAU: Tusikubali misamaha ‘duni’ kutoka kwa wanasiasa wetu waliojaa unafiki

WANDERI KAMAU: Tusikubali misamaha ‘duni’ kutoka kwa wanasiasa wetu waliojaa unafiki

NA WANDERI KAMAU

WAKATI mwingine, huwa inashangaza kutafakari ikiwa wanasiasa huingiwa na roho fulani wanapowahutubia wafuasi wao, kiasi cha kujisahau wao wenyewe.

Mtindo huu wa wanasiasa “kuomba radhi” baada ya kutoa matamshi ya uchochezi au kuyadunisha baadhi ya makundi katika jamii hauridhishi hata kidogo.

Kwa tathmini yangu binafsi, matamshi anayotoa mwanasiasa anapopewa kipaza sauti ndio uhalisia wa msimamo wake kuhusu masuala anayozungumzia.

Kwa mfano, matamshi ya Seneta Cleophas Malala (Kakamega) kwamba kazi ya polisi ni kushika na kutumia bunduki pekee ni ya kusikitisha sana. Bw Malala pia alinukuliwa akisema kuwa kinyume na taaluma nyingine, polisi hawana masomo ya kutosha.

Ijapokuwa Seneta huyo aliomba msamaha kutokana na matamshi hayo, hilo linaonyesha msimamo wake na dhana aliyo nayo kuwahusu polisi au makundi mengine katika jamii.

Kila wakati uchaguzi unapokaribia, huwa tunawaona wanasiasa wakitoa kila aina ya matamshi na baadaye kuomba radhi kutokana na athari zake katika jamii.Baadhi ya matamshi hayo ndiyo yamekuwa yakihusishwa na matatizo yaliyotukumba hapo awali nchini kama vile ghasia za baada ya uchaguzi tata wa 2007/2008.

Matamshi yayo hayo ndiyo yanahusishwa na ghasia zilizoshuhudiwa nchini mnamo 1992, 1997 na 2017.

Uchaguzi mkuu unapokaribia, wito mkuu kwa taasisi muhimu kama Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) ni kutokubali baadhi ya “misamaha” inayotolewa na wanasiasa, kwani matamshi yao yanaashiria misimamo yao halisi.

  • Tags

You can share this post!

VITUKO: Harusi tunayo! Staa Rashford avisha Lucia pete ya...

Utalii: Balala awataka wawekezaji kusaka soko jipya

T L