Wanga ajiondoa lawamani mgomo wa wahudumu

Wanga ajiondoa lawamani mgomo wa wahudumu

NA GEORGE ODIWUOR

MWAKILISHI wa Kike Kaunti ya Homa Bay, Gladys Wanga amewataka wakazi kutomwekea lawama kuhusu mgomo wa wahudumu wa afya ulioathiri sekta ya afya katika kaunti hiyo.

Alisema kuwa ofisi yake haihusiani na serikali ya kaunti na kwa hivyo hafai kuhusishwa moja kwa moja kusuluhisha matatizo yanayokumba sekta hiyo.

Aliwataka wakazi kutochanganya jukumu lake bungeni na kujaribu kuyalinganisha majukumu yake na yale ya wabunge wengine na madiwani.

Hospitali za umma katika kaunti hiyo zimefungwa kwa muda wa wiki tatu baada ya wahudumu wa afya kugoma wakidai malipo yao ya Aprili.Huduma zingine pia zimeathiriwa huku waajiriwa wengine pia wakidai malipo yao.

Hata hivyo, wakazi wanawalaumu viongozi wa eneo hilo kukosa kusuluhisha masuala hayo. Bi Wanga alisema kuwa hahusiki moja kwa moja na masuala ya serikali ya Kaunti.

“Nalaumiwa kwa kunyamanza huku wahudumu wa afya wakiendelea na mgomo. Hata hivyo, sifai kulaumiwa kwa kuwa nahusika na masula ya serikali ya juu na wala si serikali ya kaunti,” akasema Bi Wanga.

Hata hivyo, aliahidi kuleta mabadiliko katika sekta ya afya iwapo atachaguliwa gavana wa kaunti hiyo.

  • Tags

You can share this post!

Sonko apewa siku 21 kujibu kesi ya kutelekeza mtoto

IEBC yampa Kalonzo muda wa hadi Jumapili Mei 29 kuwasilisha...

T L