Wanjigi aelezea imani atambwaga Raila na kubeba bendera ODM

Wanjigi aelezea imani atambwaga Raila na kubeba bendera ODM

Na PIUS MAUNDU

MGOMBEA URAIS JIMMY Wanjigi ameelezea imani ya kumbwaga kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga katika kiny’ang’anyiro cha tiketi ya kuwania urais kwenye uchaguzi ujao.

Akizungumza jana alipokutana na wanafunzi wa vituo vya mafunzo na vyuo vikuu katika Machakos People’s Park, Mjini Machakos, Bw Wanjigi alijivunia kuungwa mkono na wajumbe zaidi ya 3, 000 wa ODM.

“Wajumbe katika kaunti 12 wameidhinisha ugombeaji wangu,” alisema akirejelea matokeo ya mkutano wake Jumatano na maafisa wa ODM kutoka maeneo ya chini Mashariki na Mlima.Maafisa hao waliunga mkono ugombea wake huku Bw Wanjigi akiitaka Bodi ya Kitaifa kufungua tena kinyang’anyiro cha tiketi ya urais kufuatia hatua ya kukifutilia mbali mnamo Februari.

“Tuna imani na demokrasia ya chama na tunajua walipo wajumbe. Jana nilikuwa na wajumbe kutoka kaunti 12 waliounga mkono uwaniaji wangu. Kaunti hizo 12 zina wajumbe zaidi ya 1500,”“Mfumo wa wajumbe ni 3000 katika ODM.

Tunajua ni wapi idadi kubwa ipo na tunaamini demokrasia ya chama ni muhimu,” alisema Bw Wanjigi.Aidha, alisema ndiye mgombea pekee anayewania tiketi ya urais ya ODM kwa sababu Bw Odinga hajatangaza wazi uwaniaji wake.

ODM ilisitisha mchakato wa kutambua mpeperushaji bendera wa chama hicho mnamo Aprili.

You can share this post!

Uingereza yaahidi kupiga jeki uchumi wa Kenya

Raila ataka Chebukati kuomba Kenya radhi

T L