Habari Mseto

Wanne waliouawa na mama yao wazikwa

July 2nd, 2020 1 min read

MACHARIA MWANGI na FAUSTINE NGILA

Watoto wanne waliouliwa na mama yao Naivasha Ijumaa iliyopita wamezikwa katika mazishi yaliokuwa na majonzi Kinangop kaunti ya Nyandarua.

Waliohudhuria mazishi hayo walishindwa kushilikia machozi yao wakati majeneza yalipokuwa yakitolewa kwenye gari.

Wakazi na wanakijiji wa Murungaru walihudhuria mazishi hayo kwa wingi huku wakikiuka mikakati iliyowekwa ili kudhibiti kusambaa kwa virusi vya corona.

Maafisa waliohudhuia walilazimika kufanya kazi kupita kiasi huku wakihakikisha kwamba umbali wa mita moja umezingatiwa.

Katika shehere hiyo makasisi waliwaomba watu ambao wanapitia mambo mangumu na msongo wa mawazo kutafuta ushauri.

“Wanapaswa kuongea na marafiki wao na jamaa na kujadiliana kuhusu matatizo wanayopitia,” alisema Francis Kamau wa Kenya Assemblies of God.

“Familia zinapitia wakati mgumu wakati huu wa janga la corona na wanaotdhirika hapaswi kunyamazia matatizo,”alisema Bw Mwaura.