WANTO WARUI: Wasimamizi wa shule za sekondari wapewe mafunzo ya uongozi bora

WANTO WARUI: Wasimamizi wa shule za sekondari wapewe mafunzo ya uongozi bora

Na WANTO WARUI

MATATIZO mengi yanayoathiri shule zetu za sekondari nchini huenda yanasababishwa na uongozi uliopitwa na wakati.

Si siri kuwa bodi za shule za sekondari aghalabu hujumlisha wazazi wakongwe wengi wao wakiwa waanzilishi wa shule hizo, ambao ndio hutegemewa katika kutoa mwelekeo wa shule hasa matumizi ya pesa. Wakati mwingine, hata mwalimu mkuu hushindwa kutoa maamuzi yafaayo kwa kuogopa mwenyekiti wa bodi.

Licha ya hayo, walimu wengi wakuu wa shule za upili wanashikilia udumishaji wa nidhamu kwa njia moja tu – ile ile tuliyoachiwa na mkoloni ya kuamrisha mambo kwa kutumia nguvu, watu watake wasitake. Ni kweli kabisa kuwa kuna baadhi ya shule za sekondari ambako walimu wakimwona mwalimu mkuu huwa wanakimbia kama watoto kwa kuogopa kufokewa au kupata ‘adhabu’.

Ikiwa mambo kama haya yapo kwa walimu, itakuwaje kwa wanafunzi?Uongozi uliopitwa na wakati huenda unachangia pakubwa katika migomo mingi inayopatikana shuleni. Wanafunzi walio shuleni sasa ni zao la teknolojia ya karne ya ishirini na moja.

Kufikiria kwao na mtazamo wao wa mambo ni tofauti kabisa na wa karne ya ishirini. Hii ndiyo sababu hata elimu ambayo wanafundishwa na mbinu zinazotumiwa kuwafundisha hazifai kuwa zile zile za karne iliyopita. Katika kutumia mbinu hizo hizo za kale za kufundishia, hapana shaka wanafunzi watakuwa wakaidi maadam hazipelekani na mahitaji ya kisasa ya maisha.

Hii ndiyo sababu ninatoa kauli kuwa wasimamizi wa shule zetu za sekondari wapewe mafunzo mwafaka ya uongozi ili wapate maarifa zaidi ya kuwawezesha kukabiliana na wanafunzi wa leo. Mpango maalum wa serikali kwa walimu wote wa sekondari unaonuiwa kuwapiga jeki katika elimu ya uongozi wa kisasa unaweza kusaidia pakubwa.

Wizara ya Elimu ina jukumu la kuhakikisha kuwa walimu wakuu wamepata mafunzo yafaayo ya usimamizi

You can share this post!

AC Milan watua kileleni mwa Serie A baada ya Atalanta...

TAHARIRI: Hawakustahili kufa namna ile katika ajali ya basi...

T L