Michezo

Wanyama asherehekea bathidei ya 29, Wakenya wamponda

June 25th, 2020 2 min read

Na GEOFFREY ANENE

Mashabiki Wakenya wamemrushia makombora Victor Mugubi Wanyama kuhusu miaka yake baada ya kugonga umri wa miaka 29 leo Juni 25, 2020.

Wamejitosa kwenye mitandao ya kijamii kumtania kuhusu umri huo wake ambao wanaonekana kutilia shaka. Wengi wanaona umri wake unafaa kuwa kati ya 30 na 46.

Wanyama amecheza soka yake ya malipo ughaibuni tangu Julai 2007 akianzia klabu ya Helsingborg (Uswidi) na kuelekea Beerschot nchini Ubelgiji kabla ya kupata umaarufu Celtic nchini Scotland na kisha kuingia Uingereza kuchezea Southampton na Tottenham kabla ya kujiunga na Montreal Impact nchini Canada mnamo Machi 3, 2020.

Nchini Kenya, Wanyama alivalia jezi za Nairobi City Stars na AFC Leopards. Wanyama anafahamika kwa majina ya utani ya Lion of Muthurwa na Big Vic.

Huku Montreal Impact ikijiandaa kurejea uwanjani Julai 9 baada ya michezo kusimamishwa nchini Canada mnamo Machi 12 kuzuia maambukizi ya virusi vya corona, haya hapa maoni ya baadhi ya Wakenya waliomtakia Wanyama siku njema ya kuzaliwa kwake.

Rodgers Podolski Evayo anasema: Happy birthday The Big Vic as you turn 26 in Europe, 30 in America and 46 in Kenya, anyway it’s none of my business, just wishing you healthy, happy and successful moments Omwami…”

Tony Thiery: Happy birthday bro as you turn 46… There’s no way I am older than you and you started playing for Harambee Stars when I was in lower classes.

Joy Tesh: Happy birthday Vic keep soaring Kenya flag in soccer…seems your age has become people’s disease whether 46 or 26 the effort is all the same.

Githinji Gitau: He has multiple birthdays in one calendar and a stagnant age. And Victor’s God will be my God.

Slims Koinange: How old is he 35, 38 never mind, Happy birthday to him.

Wil Omondi: He’s turning 28 in Europe but here in Kenya his younger sister is turning 36. HBD

Abdimalik Said: Happy 43rd to Victor Wanyama. Age gracefully.

Khamisi Acadius Mukoto: Happy birthday mukhuvi, sorry Mugubi… Under 30 forever!

Hillary Kihuga: Yeah, he turns 37 but we don’t say it loudly since at Spurs they know he’s now 28.