Habari Mseto

Waombolezaji 25 kutoka Mombasa wazuiliwa Siaya

June 13th, 2020 1 min read

NA DICKENS WESONGA

Waombolezaji 25 waliosafiri kutoka Mombasa hadi Siaya kuhudhuria mazishi walizuiliwa na kutengwa Ijumaa.

Mkuu wa polisi Antony Wafula alisema kwamba waombolezaji hao walikamatwa kwa sababu ya kutotoa stakabathi zilizoonyesha kuwa walikuwa wamepimwa virusi vya Corona Bondo walisema kwamba Bondo.

Polisi waliruhusu hafla ndogo ya mazishi ya Evans Odongo kabla ya kuwakamata waombolezaji hao na kuwapeleka kwenye kituo cha kutenga wagonjwa cha Chuo cha Mafunzo ya Udaktari cha Siaya.

Anne Wekesa, mjane wa Odongo na watoto wake watatu ni mmoja wa wale waliotengwa.

Bi Wekesa aliambia Taifa Leo kupitia njia ya simu kwamba bwanake aligonjeka miaka kumi iliyopita. Bw Evan alifariki Juni alipokuwa akipokea matibabu.

Bi Wekesa alisema kwama chifu kutoka Tononoka, Mombasa aliwapa barua ya kuwaruhusu kusafiri pamoja na mwili hadi Busia kwa mazishi hayo.

Mwezi uliopita Gavana wa Siaya Cornell Rasanga aliomba familia zitakazopoteza watu wao wakiwa Nairobi ama Mombasa wawazike huko.

Hii ni baada ya waombolezaji wengine kulisafiri kutoka Kibra kumzika mwanamke aliyefariki kutokana na corona kupatikana na virusi hivyo.