Habari Mseto

Wapatikana wamefungua chuo wakati vyuo vimefungwa

August 25th, 2020 1 min read

Na Gastone Valusi

MAAFISA wa kushughulikia maswala ya corona katika Kaunti Ndogo ya Yatta ilifunga kituo cha ufundi cha kibinafsi kwa madai kwamba chuo hicho kilikiuka mikakati iliyowekwa na serikali ya kupambana na virusi vya corona.

Naibu Kamishna wa eneo hilo Bw Joseph Mukururi ambaye pia ni mwenyekiti wa maafisa hao alisema kwamba chuo cha kiifundi na technologia cha Kilimambogo kilisemekana kufungua Agosti 15 kinyume na maelekezo ya serikali kwamba vyuo vya ufundi vitafunguliwa Januari 2021.

“Tumefunga kituo hicho cha ufundi kwa kukiuka maelekezo ya serikali na uchunguzi unaendelea kubaini ni kwa nini chuo hicho kilifungua. Usimamizi wa chuo hicho unahatarisha maisha ya wanafunzi, walimu na majirani wanaoishi karibu na chuo hicho na hatuwezi kuruhusu hayo,” alisema.

Bw Mukururi alisema kwamba chuo hicho kilikuwa na wanafunzi 61 na wafanyakazi 9 wakati kilifungwa.

Alionya kwamba  maafisa wa vyuo vinavyopanga kufungua wqkamatwa na kushtakiwa.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA