Habari Mseto

Wapenzi wasema walimuua mtoto kuokoa uhusiano wao

September 29th, 2020 1 min read

NA TITUS OMINDE

Wapenzi wawili kutoka Kijiji cha Cherus Kaunti ya Uasin Gishu wameshatakiwa kwa mauaji ya mwana wao wa miaka mitatu aliyeuwa na ulemavu na kumuzika kwenye kichaka cha Singalo kisiri.

Charity Cheruto mwenye miaka 21 na Timoth Lihanya wa miaka 28 walisema walimuua mtoto huyo ili kuokoa mapenzi yao.

Chifu wa Olunguse Samuel Bitok alisema kwamba alishuku alipata habari kuhusu kupotea kwa msichana mmoja. Alisema alisema kwamba wawili hao walianza kuonekena wenye wasiwasi baada ya kuulizwa kuhusu mtoto wao.

“Walisema kwamba mtoto huyo alikuwa amepelekwa kwa jaamaa yake lakini sikuhamini Habari hiyo kwa hivyo nilisisitiza niambiwe ukweli,” alisema Bw Bitok.

“Nilisisitiza niambiwe ukweli kuhusu mahala mtoto huyo yuko.Hapo ndipo mama yam toto alikiri kwamba walimuua na wakamzika kwenye kichaka”.

Hapo ndipo chifu huyo aliwaangiza wawili hao wamwonyeshe kaburi hilo.Baadaye walipelekwa kwenye kituo cha polisi cha  Kondoo.

Polisi walisema kwamba wawili hao waliua msichana huyo tarehe 20 Septemba na kuuzika mwili wake kichakani saa mbili usiku.

Wawili hao walishtakiwa  kwa mauaji Eldoret Jumatatu.

Majirani walisema kwamba wawili hao walikuwa wanafanya kazi ya vibarua sokoni na kwamba walikuwa wanafungia wanamgungia kwa nyumba kila walipokuwa wakienda kazini.