Kimataifa

Wapigakura wakerwa na ANC kura zikiwadia

May 28th, 2024 2 min read

NA MASHIRIKA

JOHANNESBURG, AFRIKA KUSINI

UCHAGUZi mkuu nchini Afrika Kusini utafanyika Jumatano huku raia wakighadhabishwa na kupotea kwa nguvu za umeme mara kadhaa, ukosefu wa ajira na kukithiri kwa ufisadi.

Wapigakura watapiga kura siku hiyo wakitishia kumaliza utawala wa chama cha African National Congress (ANC), kilichotamalaki taifa hilo kwa miaka 30 baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Nelson Mandela kuongoza akiwa ndani ya ANC.

Hakuna wakati wowote, tangu vyombo vya habari duniani kuonesha picha za wapigakura wa Afrika Kusini wakipanga foleni kupiga kura kwa mara ya kwanza kufuatia kumalizika kwa utawala wa Weupe walio wachache, ambapo chama cha ANC kimeonekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kupoteza wingi wake wa wabunge.

Kura za maoni zinaonyesha kuwa sehemu ya ANC ya kura inaweza kushuka hadi asilimia 40, ikilinganishwa na asilimia 57.5 katika mwaka wa 2019, ambayo ingelazimisha chama hicho kuingia katika muungano mbaya na wapinzani – na uwezekano wa kumuweka Rais Cyril Ramaphosa kwenye changamoto ya uongozi.

Hata hivyo, utafiti uliotolewa mapema wiki hii na kampuni ya kufanya tafiti, Afrobarometer ulionesha kwamba theluthi moja ya wapiga kura walikuwa hawajaamua, na kufanya uchaguzi huu kuwa usiotabirika zaidi katika historia ya kidemokrasia ya Afrika Kusini.

Kulingana na mtafiti wa masuala ya siasa katika Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Nicole Beardsworth anaona ANC ikipata “pigo dogo” siku hiyo, na kutatanisha utabiri mbaya zaidi – hasa kwa kuanzishwa na Ramaphosa mwezi huu kwa kufanya ahadi maarufu kama vile sheria ya bima ya afya ya kitaifa na kupendekezwa kwa ruzuku ya msingi ya mapato.

“Lakini sidhani kama tutaona ANC ikipata zaidi ya asilimia 50,” alisema.

“Wao … watakuwa wakijadiliana kuhusu kufanya muungano na wanachama kutoka vyama vingine. Swali kubwa ni, na nani?”

Mtafiti huyo alisema mengi itategemea jinsi wanavyofanya mambo yao, aidha kwa kuyafanya vizuri au vibaya.

Kiwango kidogo kitawawezesha kufanya makubaliano na kuungana na chama kingine chenye uwezo mdogo wa kufanya mahitaji muhimu.

Kupoteza wafuasi zaidi kunaweza kumaanisha kuungana na chama cha Marxist Economic Freedom Fighters (EFF) – matarajio ambayo yanawafanya viongozi wa biashara na wazungu wachache wa Afrika Kusini kutetemeka – au na vyama kadhaa vidogo ambavyo vinaweza kuvuruga majadiliano ya kufanya maamuzi.