Warembo wa Brazil wazamisha Colombia na kutawazwa malkia wa Copa America

Warembo wa Brazil wazamisha Colombia na kutawazwa malkia wa Copa America

Na MASHIRIKA

PENALTI ya Debinha de Oliveira iliwazolea warembo wa Brazil taji la Copa America kwa mara ya nne mfululizo baada ya kukomoa wenyeji Colombia 1-0 mnamo Jumapili mjini Bucaramanga.

Pia Sundhage sasa ndiye kocha wa kwanza mwanamke kuwahi kunyanyua taji hilo ambalo Brazil wametwaa mara nane kutokana na makala tisa yaliyopita.

Chini ya Sundhage, Brazil walifunga mabao 20 kutokana na mechi sita za makala ya mwaka huu huku wapinzani wakishindwa kabisa kutikisa nyavu zao. Ushindi huo uliwazolea tuzo ya Sh178.5 milioni huku Colombia wakitia kapuni Sh59.5 milioni.

Ufanisi huo wa Brazil na Colombia kwenye Copa America umewakatia tiketi za kunogesha fainali za Kombe la Dunia 2023 na Michezo ya Olimpiki itakayofanyika jijini Paris, Ufaransa mnamo 2024.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wakuu wa kaunti washtakiwa kwa wizi wa Sh17.9 milioni

Vipusa wa Uingereza wapiga Ujerumani na kutwaa taji la Euro...

T L