Habari Mseto

Washangaa kupata mwili uliochomwa wa mwanamke chumbani kwake

November 8th, 2020 1 min read

DERRICK LUVEGA NA FAUSTINE NGILA

Wakazi wa Kaunti ya Vihiga walipigwa na butwaa baada ya mwanamke wa miaka 20 kupatikana akiwa amefariki nyumbani kwake huku mwili wake ukiwa umechomwa.

Naibu chifu wa Demesi Bw  Oscar Jumba alithibitisha  kisa hicho Alhamisi jioni. Mtoto wa kike wa wiki mbili alikimbizwa hospitali huku ripoti zikisema kwamba alikuwa amejaza mapafu kwa moshi.

Kilichosababisha kifo cha Esther Musimbi ambaye alijifungua kwa njia ya upasuaji wiki mbili zilizopita  hakijulikani.

Alipo mmewe mwathiriwa Maxwel Adembesa wa mika 24 hapajulikani .Bw Adembesa alikuwa ameondoka Jumanne usiu kabla ya kisa hicho..

Lakini hakupatikana baada ya wakati kugundua moshi ukitokea nyumbani kwao amabayo ilikuwa imefungwa na ndani.

Naibu chifu wa eneo hilo alipashwa Habari hiyo na majirani ambao walivunja nyumba hiyo na kuingia ndani ambapo walipata mwili wa mwanamke huyo na mtoto huyo wa wiki mbili.kisu kilipatikana shingoni mwa mwanamke huyo.

“Majirani waliona moshi ukitoka nyumbani kwao iliyokuwa imefungwa kutoka na ndani wakapta mtoto aliyekuwa akilia nah uku akipambana kupumua mamayake alikuwa tayari ameshafariki,”alisema Bw Jumba.

Naibu chifu alijulisha maafisa wa polisi kutoka kituo cha polisi cha Kilingi ambao walikimbia kwenye eneo la tukio huku uchunguzi ukiendelea.

“Mwanamke huyo alikuwa amejifungua wiki mbili zilizopita na mumewe hajaonekana kwa muda wa siku tatu.Tunambiwa alikuwa mumewe alikuwa nyumbani Jumatano usiku,”alisema Bw Jumba.

Mwili wa mwathiriwa ulipelekwa kweenye chumba cha kuhifadhi mairi cha hospitali ya Vihiga.