Washirika wa Raila Magharibi wamrai Kalonzo kurudi Azimio

Washirika wa Raila Magharibi wamrai Kalonzo kurudi Azimio

NA SHABAN MAKOKHA

WASHIRIKA wa mgombea urais wa Azimio Umoja One Kenya, Raila Odinga eneo la Magharibi, wamemrai kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka kubadilisha nia na kurejea katika muungano huo.

Mbunge wa Lugari Ayub Savula, Mwakilishi Mwanamke wa Kaunti ya Kakamega Elsie Muhanda na mgombea ugavana wa kaunti hiyo wa chama cha ODM Fernandes Barasa walimuomba Bw Musyoka kutogombea urais kivyake.

Wiki iliyopita Bw Musyoka alitangaza kujiondoa katika muungano wa Azimio kugombea urais kwa tikiti ya Wiper alipokosa kuteuliwa mgombea mwenza wa Bw Odinga, ambaye badala yake alimteua Kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua.

  • Tags

You can share this post!

Urusi yalipiza kwa vikwazo vya Biden

Karua afufua Raila katika Mlima Kenya

T L