Habari Mseto

Washtakiwa kupatikana na bandi ya mamilioni

August 18th, 2020 1 min read

Na Richard Munguti

Washukiwa wanne wa mihadarati miongoni mwao raia wa Uganda walishtakiwa Jumanne kwa kasafirisha bangi iliyo na thamani ya Sh11.5 milioni.

Raia wa Uganda Stephen Wandera Baraza mwenye umri wa miaka 35 na raia wa Kenya Tom Ouma Aero,48 na Paul Ochieng Otieno aliye na umri wa miaka 35 walishtakiwa katika mahakama iliyoko uwanja wa ndege wa JKIA.

Mshtakiwa wa nne Ruth Otieno hakufika kortini kama alivyokuwa ameagizwa na afisa mkuu kituo cha polisi cha Shauri.

Mahakama ilielezwa na mshtakiwa huyo wa nne alitakiwa afike kortini Jumanne lakini hakufika.

Mahakama iliombwa itoe kibali cha kumkamata Ruth lakini wakili Danstan Omari akapinga akisema atamfikisha mahakamani Jumatano.

Hata hivyo hakimu aliamuru kesi itajwe Agosti 19 ndipo polisi wakamilishe uchunguzi…

Washtakiwa hao watatu waliachiliwa kila.mmoja kwa dhamana ya Sh500000.

“Naomba nipewe muda nimfikishe Ruth Atieno Ouma Jumatano.

“Naomba hii korti iwaachilie kwa dhamana washtakiwa waliofikishwa mahakamani waachiliwe kwa dhamana,” Omar.

Aliachiliwa kwa dhamana ya Sh2 milioni na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho.

Walishtakiwa kupatikana na bhangi hiyo mnamo Agosti 14 2020 katika kituo cha kupima uzani kilichoko Gilgil.

Wanne hao walidaiwa walisafirisha bhangi hiyo wakitumia gari la kibinafsi.