Habari Mseto

Washukiwa 14 wa ghasia kuzuiliwa kwa siku 10

August 8th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Korti ya Nakuru imeagiza washukiwa 14 waliokamatwa kufuatia vita vilivyoshuhuhudiwa kwenye kaunti ndogo ya Njoro wiki iliyopita wazuliwe kwa siku 10 ili waruhusu polisi kufanya uchunguzi.

Hakimu mkuu Elizabeth aligiza kwamba washukiwa hao wakiwemo diwani wa Nessuit Joseph Miangari na afisa wa usalama wazuiliwe kwenye kituo cha polisi cha Bondeni na Njoro.

Polisi walisema kwamba walikuwa wanachunguza mauaji, vita na uchochezi wa kuzua vurugu.

Bw Tobolei alisema kwamba walikuwa wanahitaji muda ili wakamilishe uchunguzi. Washukiwa hao walikamatwa Ijumaa kufuatia ghasia ziliozuka Jumatano.

Hakimu alisema kwamba washukiwa hao wafikishwe kortini Agosti 13.