Habari Mseto

Washukiwa 9 wa Kenya Power wasakwa na DCI

August 25th, 2018 1 min read

Na BERNARDINE MUTANU

Wachunguzi wa uhalifu wanawatafuta washukiwa tisa wanaohusishwa wizi na uuzaji wa mali ya kampuni ya umeme ya Kenya Power.

Idara ya Uhalifu (DCI) Ijumaa ilisema washukiwa hao wa Catherine Wanjiko Njuguna, Christine Nyawara na Edwin Machaira Ngamini wote wa Mallous Enterprises, na John Waweru wa Kazimix Enterprises, wanashukiwa kutekeleza uhalifu huo.

Wengine ni Jason Morara, James Ongechi, Jeremiah Onduko wote wa Jake Building and Construction Limited, Stephen Njoroge Maina wa Wachema Investments Limited na Bi Linet Njeri wa Pestus Investments Limited.

Mahakama moja ya Nairobi ilitoa agizo la kukamatwa kwao. DCI sasa inataka wananchi kuisaidia kuwapata iliwaweze kufunguliwa mashtaka.

Kulingana na idara hiyo, yeyote aliye na habari kuwahusu anafaa kuripoti katika Mahakama ya Milimani ya kukabiliana na Ufisadi No.1 au katika afisi ya DCI.