Habari Mseto

Washukiwa waliokamatwa na nyama ya twiga Garissa wanashtakiwa leo

June 15th, 2020 1 min read

Na FARHIYA HUSSEIN

WASHUKIWA wanne ambao walinaswa na nyama ya twiga wanashtakiwa leo Jumatatu katika mahakama ya Garissa.

Wanne hao walikamatwa katika eneo la Ijara kwa kumiliki nyama ya twiga kwa njia zisizofaa.

“Maafisa kutoka Shirika la Huduma kwa Wanyamapori ya Kenya, Northern Rangelands Trust na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai walipata kilo 150 za nyama ya twiga baada ya watuhumiwa hao wanne kukamatwa,” imesoma sehemu ya taarifa ya KWS.

Taarifa hiyo ilionyesha zaidi kuwa watuhumiwa hao walipatikana na vifaa vya uwindaji na pikipiki.

Walizuiliwa katika kituo cha polisi cha Masalani mnamo wikendi wakisubiri mashtaka ya umiliki wa nyama kiharamu.