Washukiwa wawili wakamatwa kwa kuuza pombe haramu na mihadarati mtaani Mukuru-Reuben

Washukiwa wawili wakamatwa kwa kuuza pombe haramu na mihadarati mtaani Mukuru-Reuben

NA SAMMY KIMATU

WASHUKIWA wawili wa uhalifu wa kuuza pombe haramu na mihadarati na ambao polisi wanasema wamekuwa mafichoni kwa muda mrefu hatimaye wamekamatwa.

Kamanda wa polisi eneo la Makadara, Bi Judith Nyongesa alisema alishirikiana na mkuu wa kitengo cha uhalifu wa Jinai, Bw Felix Nyamai Kithuku kuweka mtego ndiposa wakafanikiwa kuwanasa wawili hao.

Bi Nyongesa alisema Bi Devina Kerubo amekuwa akiendesha biashara ya kuuza pombe haramu ya chang’aa na akikamatwa, polisi walinasa lita 50 za pombe hiyo zikiwa zimefichwa.

Isitoshe, mshukiwa wa pili, Bw Stephen Nyasimi alikamtwa kwa kuuza chang’aa na mihadarati.

Polisi wanasema alikamtawa akiwa na misokoto 100 ya bangi na lita tatu za chang’aa.

Kadhalika, wawili hao huendesha biashara yao katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Reuben ulioko katika kaunti ndogo ya Embakasi Kusini.

“Wawili hawa wanalaumiwa na wakazi kwa kuchangia pakubwa katika uhalifu huku wakishukiwa kwa kuwaficha wahalifu na kuharibu maisha ya vijana na ndoa kusambaratika wazee wakilewa chakari,” Bi Nyongesa akasema.

Bi Nyongesa alishauri wananchi kutumia pombe zilizoidhinishwa na serikali na kuwaomba wafanyabiashara kuwa na leseni za uuza pombe.

“Bali na kuwa na leseni za kufungua baa na maeneo mengine ya burudanimni lazima sheria ya saa na wakati wa kufungua vilabu ziambatane kwa mujibu wa sheria. La sivyo, tutakuja kukukamata,” Bi Nyongesa asema.

Bw Nyamai alisema maafisa wake wako mbioni kuwahoji washukiwa hao ili wasaidie kuwakamata washukiwa wanaotumia baa zao kama maficho kabla na baada ya kufanya uhalifu.

Hayo yakijiri, Bi Nyongesa alisema usalama ulikuwa umeimarishwa kabla, wakati na baada ya msimu wa sherehe mnamo Disemba mwaka jana.

Aliongeza kwamba mikakati kambambe waliyopanga na Bw Nyamai yalifanikisha juhudi zao kuzaa matunda.

Bi Nyongeza aliongeza kwamba alitumia maafisa wake wanaovalia sare na kushirikisha maafisa kutoka kwa Bw Nyamai na kikosi mmalumi cha SPIV.

“Tulikuwa mna ,seto wa polisi waliovalia kiraia na wenzao waliovalia zare zao na pia muwashirikisaha maafisa wetu wa SPIV kando na kuimarisha ushikaji doria barabarani, mitaani na maeneo yaliyokuwa hatari kwa watu kutembea miguu usiku na mchana,” Bi Nyongesa akanena.

Vilevile, anawapongeza  wanakamati wa Nyumba Kumi na wananchi kwa kushirikiana na polisi kutoa habari zinazohusiana na masuala ya usalama.

Kadhalika, kamanda Nyongesa, anapongeza ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome kwa kuongezea kaunti ndogo ya Makadara vituo vitatu vipya.

Zaidi ya hayo, amewaongezea kambi za polisi bambazo anasema zimepiga jeki usalama wa raia na wakazi kwa ujumla.

  • Tags

You can share this post!

Clevers Kyalo: Kiungo mahiri mwenye ndoto ya kuchezea...

SHINA LA UHAI: Kisonono chaweza sababisha utasa na athari...

T L