Habari Mseto

Wasichana 28 hupachikwa mimba kila siku Machakos – Utafiti

June 17th, 2020 1 min read

NA MWANDISHI WETU

Zaidi ya wasichana 28 hupata ujauzito kila siku katika kipindi cha miezi mitano iliyopita Kaunti ya Machakos kulingana na utafiti uliofanywa na Mfumo wa Habari za Afya nchini. 

Utafiti huo ulionyeshwa kwamba wasichana 3,964 wenye miaka isiyozidi 19 waliripotiwa kupata mimba wakati huo.

Athi River ndio  mtaa wenye visa vingi zaidi huku eneo la Kalama likiwa na visa vichache za mimba za wasichana wa shule kulingana na data iliyotolewa hospitalini na kuonekana na Taifa Leo.

Visa hivyo viliongezeka Machi. Afisa wa Watoto Machakos Salome Muthama alisema kwamba visa hivyo vikikuwa vichake kuliko idadi hiyo.

Idadi hiyo inatarajiwa kupanda zaidi kutokana na janga la corona .

“Visa vingi vitatokana na watoto waliotolewa mijini na kuletwa kuishi na nyanya zao kutokana na janga la corona huku wazazi wakirudi kuishi mijini,” Bi Muthama aliwaabia wanahabari mjini Machakos..