Habari Mseto

Wasichana 80 wakosa shule sababu ya tohara

October 16th, 2020 1 min read

NA IAN BYRON

Wasichana 80 kutoka Kuria Magharibi bado hawajarudi shuleni kwani walitoroka makwao wakihofia kukeketwa.

Wanafunzi hao walijificha Shule ya Upili ya Taranganya wakati msimu wa kutahiri ulifika wa jamii ya Wakuria huku jambo hilo likiathiri shughuli za masomo eneo hilo.

Wasichana walio na umri wa miaka kati ya  tisa na 13 ndio wanalegwa kwenye shugli hiyo ya kutahiri huku  serikali ikiwatafuta wanaoendesha shugli hiyo haramu.

*Teresia (Sio jina lake) alitorokea kwenye kambi hiyo Jumatatu wakati shule zilifunguliwa baada ya kupata habari kwamba wazazi wake walikuwa wanataka atairiwe.

“Shangazi yangu aliniarifu kuhusuiana na mipango ya kutairiwa na akanisaindia kutorokea kituo cha polisi cha Kehancha baada ya kugundua kwamba nilikuwa nitairiwe,”alisema msichana huyo wa miaka 14.

Anahofia kwamba masomo yake yatakatizwa baada ya baba yake kumkana kwasababu ya kukataa kutairiwa.

“Nahofia kwamba wazazi wangu hawataki mamabo yangu kama sitakeketwa nagoja kufanya mtihani wangu wa KCPE lakini nikienda nyumbani itakuwa lazima nikeketwe,” alisema.

Kati ya hao 80 walioko kwenye kituo hicho 20 ni wa darasa la nane huku sita wakiwa wa darsa la nne.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA