Wasichana wazidi idadi ya wavulana katika KCSE Kwale

Wasichana wazidi idadi ya wavulana katika KCSE Kwale

Na Valentine Obara

KAUNTI ya Kwale ni miongoni mwa kaunti 15 kitaifa zilizokuwa na pengo kubwa la idadi ya wasichana kuliko wavulana waliofanya Mtihani wa Kitaifa wa Shule za Upili (KCSE) wa 2020.

Katika matokeo ya mitihani yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu, Prof George Magoha, Kwale pamoja na Taita Taveta pekee ndizo kaunti za Pwani zilizokuwa katika orodha hiyo.

Kaunti nyingine kwenye orodha hiyo ni Nyandarua, Nyeri, Kirinyaga, Murang’a, Kiambu, Machakos, Kitui, Meru, Nandi, Elgeyo Marakwet, Kakamega, Vihiga and Kisumu.

Kwale huwa ni miongoni mwa kaunti ambazo hutajwa mara kwa mara kuwa na idadi kubwa ya wasichana wanaoshika mimba wakiwa wangali wanafunzi wa shule za msingi na upili.

Kwa upande mwingine, kaunti ambazo ziliibuka kuwa na pengo kubwa la idadi ya wavulana kuliko wasichana ni Mandera, Wajir, Garissa, Turkana na Homa Bay.Waziri aliagiza maafisa kuchunguza chanzo cha hali hiyo. Kulikuwa na watahiniwa 380,327 wa kiume na 366,834 wa kike.

 

You can share this post!

Watahiniwa watumia mbinu mpya za wizi KCSE

Historia matokeo yakitua siku 3 baada ya usahihishaji