Wataalam sasa wataka wanafunzi wa umri wa miaka 15 kupatiwa kondomu na dawa za kuzuia mimba

Wataalam sasa wataka wanafunzi wa umri wa miaka 15 kupatiwa kondomu na dawa za kuzuia mimba

Na WINNIE ATIENO

WATAALAM wa Afya na washikadau katika sekta hiyo wameisihi serikali kuanza kuwapa wanafunzi ambao wanaojihusisha na ngono za mapema dawa za kuzuia mimba na mipira ya kondomu ili kujikinga na maambukizi ya maradhi ya zinaa na mimba za mapema.

Kadhalika, wameisihi serikali kuwaruhusu wanafunzi ambao wamedhulumiwa kingono ikiwemo kubakwa au kunajisiwa kuavya mimba hizo.

“Wasichana wanafaa waweze kupokea dawa za kuzuia mimba, kuruhusiwa kuavya mimba na elimu ya ngono. Nchini Kenya, kuna utata kuhusu maswala ya umri kamili ambao vijana wanajihusisha na ngono lakini takwimu za Wizara ya Afya zinaonyesha kuna wengine chini ya umri wa miaka 15 wameanza kujihusisha na ngono. Kwanini tusiwape dawa za kuzuia mimba?” aliuliza Bi Ruth Mbone, mtetezi wa afya na maswala ya jamii.

Wakiongea kwenye kongamano lao la kujadili madhara ya janga la corona dhidi ya vijana huko Mombasa, walisema vijana wakipata kondomu na dawa za kuzuia mimba, serikali itaweza kudhibiti mimba za mapema miongoni mwa wanafunzi.

Dkt Angela Akol, afisa mkuu wa Ipas Africa Alliance, shirika linalojihusisha na maswala ya afya ya uzazi miongoni mwa kina mama nchini Kenya na Uganda alisema janga la corona liliathiri sekta ya afya hasa huduma.

  • Tags

You can share this post!

Uhuru ajipanga asitikiswe na Karua Mlimani

Ruto, Raila walenga kudhibiti mabunge

T L