Wataalamu wanaonya dhidi ya kutumia tembe za P2 kiholela

Wataalamu wanaonya dhidi ya kutumia tembe za P2 kiholela

Na Leonard Onyango

ILI kuepuka ujauzito, wasichana na wanawake wa umri mdogo wamekuwa wakitumia tembe za Postinor-2, maarufu kama P2, kuepuka kupata mimba baada ya kushiriki mapenzi bila kinga.

Tembe hizo zinapatikana kwa urahisi na zinauzwa kwa Sh100 madukani.Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), tembe hizo zina uwezo wa kuzuia mimba kwa asilimia 95 iwapo zitamezwa ndani ya saa 72 baada ya tendo la ndoa bila kinga.

Aidha zina madini ambayo husababisha mbegu za kiume kuwa dhaifu na kushindwa kupenya kwenye yai. Hata hivyo kutumia P2 hakumzuii mtumiaji kutokupata magonjwa ya zinaa.

Shirika la WHO linasema kuwa tembe hizo zikimezwa mara kwa mara zinaweza kutatiza hedhi.Mara nyingi anayetumia dawa hizi mfululizo anaweza kupata mvurugano wa hedhi; ikakata au akapata mfululizo na hata kuchukua muda mrefu kushika mimba pale atakapohitaji kwa sababu ya ule mvurugano wa kalenda.

WHO linasema kuwa tembe hizo hazifai kutumiwa kama njia pekee ya kuzuia mimba – watumiaji wanafaa kuwa na mbinu zingine.

 

You can share this post!

DKT FLO: Chunusi sehemu ya siri ni tatizo la kiafya?

CHARLES WASONGA: IEBC iruhusu Wakenya wote walio ughaibuni...