Wataalamu waunga Muthama ugavana

Wataalamu waunga Muthama ugavana

NA STEPHEN MUTHINI

WASOMI, wataalamu na viongozi wa wanawake kaunti ya Machakos sasa wamemuunga mkono mwenyekiti wa chama cha United Democratic Alliance Johnson Muthama kugombea ugavana kaunti ya Machakos baada ya kumteua Profesa Faith Muli kuwa mgombea mwenza wake.

Bw Muthama alimtangaza rasmi mwanapatholojia huyo katika hafla iliyofanyika katika kanisa la African Brotherhood Church Kangondi, Vyulya kaunti ndogo ya Mwaka Jumamosi iliyopita.

Dkt Mumo Matemu aliyehudhuria hafla hiyo alisema kwamba wanashirikiana na Profesa Muli na kwamba watu wa Machakos wako na bahati kwamba amekubali kushirikiana na Bw Muthama.

“Katika sekta ya elimu tuko na Faith na katika siasa na maendeleo tuko na Muthama. Faith anaungwa na wasomi wote eneo hili,” alisema Dkt Matemu.

Wasomi wengine waliounga tikiti ya Muthama na Faith Muli ni Profesa Emmanuel Mutisya, Dkt Matheaus Kauti na Dkt Mwaya Wa Kitavi anayegombea kiti cha ubunge cha Kathiani.

“Viongozi wanajulikana kwa msimamo wao kuhusu masuala na Bw Muthama ana msimamo thabiti,” akasema Dkt Kitavi.

Bw Muthama alisema kwamba ataita mkutano mkubwa wa viongozi kuamua mwelekeo wa kisiasa wa jamii ya Wakamba.

  • Tags

You can share this post!

Kindiki sasa aamua kujiondoa katika siasa baada ya uchaguzi...

Zogo wafuasi wa UDA na ANC wakilumbana

T L