Habari Mseto

Wataka Sh120,000 kwa kila ng'ombe aliyegongwa na gari

September 28th, 2020 1 min read

NA MACHARIA MWANGI

Shughuli za uchukuzi  zilikatizwa kwa saa kadhaa kwenye barabara ya Narok kuelekea Maai Mahiu  Ijumaa baada ya wakazi kufunga barabara hiyo..

Wakazi hao walilalamikia kuuliwa kwa ng’ombe wao watatu waliogongwa na gari  kwenye barabra hiyo.

Kulingana na shahidi mmoja, ng’ombe hao waligongwa na lori la changarawe Ijumaa asubuhi .Wakazi hao waliomba kufidiwa ngo’ombe hao kila mmoja, Sh120,000 kwa kila ng’ombe.

Naibu Kamshena wa eneo hilo Dennise Diffu alisema polisi wanajaribu kutataua swala hilo.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA