Habari Mseto

Wataka wafidiwe Sh10,000 kwa kila kondoo aliyeuawa na gari

October 18th, 2020 1 min read

NA GEORGE SAYAGIE

Mamia ya magari yalikwama eneo la Ntuele Narok Mashariki baada ya lori kugonga kundi la kondoo. Kufuati tukio hilo wakazi waliandamana kulalamika wakifunga barabara hiyo kwa miti na mawe.

Wakazi hao walitaka kufidiwa kondoo hao waliokufa. “Tunataka kondoo mmoja tulipwe 10,000, hatutafungua barabara hii kama hatujalipwa,” alisema mmoja wa waandamanaji.

Walisema kwamba eneo hilo ni la wafungaji na kwamba madereva wanapaswa kuendesha gari wakiwa makini.

Wakazi walisema kwamba dereva huyo alikuwa akiendesha gari akielekea Narok kutoka Nairobi alipogonga kondoo hao. Dereva huyo aliripoti kisa hicho kwenye kituo cha polisi cha Ntuele tukio hilo lilipotokea.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA