Habari Mseto

Watano kati ya 7 watiwa nguvuni Homa Bay

August 16th, 2018 1 min read

NA PETER MBURU

WASHUKIWA watano kwenye sakata ya upujaji wa Sh26 milioni katika kaunti ya Homa Bay tayari wametiwa nguvuni na wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Homa Bay.

Tano hao ambao wanajumuisha maafisa wa bunge la kaunti hiyo na waliokuwa wafanyakazi wa kaunti ni Michael Owino Ooro (aliyekuwa kiongozi wa wengi bungeni), Ouso Nyandege (aliyekuwa kiongozi wa wachache), Judith Akinyi Omogi (aliyekuwa mwanachama wa bodi ya uajiri ya kaunti), Edwin Omondo (karani) na Caroline Sang (mkuu wa kitengo cha fedha).

Maafisa wawili bado hawajatiwa nguvuni huku Mkuu wa Mashtaka ya Umma (DPP) Noordin Haji akiagiza washukiwa wote washtakiwe.