Habari

Watano watemwa Migne akitaja kikosi cha Afcon

June 11th, 2019 1 min read

Na CECIL ODONGO

KOCHA wa Timu ya Taifa Harambee Stars, Sebastien Migne, Jumanne alitaja kikosi cha wachezaji 23 kitakachowakilisha taifa kwenye kipute cha Mataifa Bingwa Barani Afrika (Afcon) nchini Misri.

Migne aliwatema wachezaji watano: Christopher Mbamba, Clifford Miheso, Anthony Akumu, Brian Mandela na Nicholas Kipkurui.

Mbamba alitemwa kwasababu ya kukosa kupona jeraha la kinena alilopata wakati wa mechi dhidi ya Madagascar. Majeraha pia yalichangia kuwaachwa nje kwa Brian Mandela.

Clifford Miheso na Anthony Akumu walitemwa kutokana na kutomridhisha mkufunzi na benchi la kiufundi.

Hata hivyo naibu nahodha Musa Mohamed na beki Aboud Omar ambao pia walipata majeraha madogo wakati wa mechi ya kirafiki dhidi ya Madagascar wamejumuishwa kwenye kikosi cha mwisho.

Harambee Stars itacheza mechi ya mwisho ya kirafiki dhidi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo(DRC) Juni 15 jijini Madrid Uhispania kabla ya kuondoka Juni 19 kuelekea Misri kwa mashindano hayo yatakayodumu kwa mwezi moja.

Mechi ya ufunguzi kwa vijana wataifa itakuwa Juni 24 dhidi ya Algeria, ambayo itachezwa siku ya tano baada ya wao kuwa kwamba watakuwa wameshawasili nchini humo.

Kikosi

Makipa: Patrick Matasi, John Oyemba, Faruk Shikalo

Walinzi: Philemon Otieno, Abud Omar, Bernard Ochieng, Musa Mohammed, Joash Onyango, Joseph Okumu, David Owino, Eric Ouma

Kiungo: Victor Wanyama, Dennis Odhiambo, Erick Johanna, Ayub Timbe, Francis Kahata, Ismael Gonzalez, Ovella Ochieng, Paul Were, Johanna Omollo

Washambulizi: Masud Juma, Michael Olunga, John Avire