Habari Mseto

Watano wazuiliwa kuhusiana na mauaji ya askari gereza

March 17th, 2024 1 min read

NA ERIC MATARA

POLISI katika eneo la Kilgoris, Kaunti ya Narok wanaendelea kuzuilia washukiwa watano kuhusiana na mauaji ya askari wawili wa magereza nyumbani mwa mwenzao aliyestaafu.

Wawili hao waliuawa nyumbani mwa afisa mstaafu Pius Limiso Ndiwa.

Walionyakwa Jumamosi, Machi 16, 2024 kuhusiana na mauaji hayo ni mkewe Bw Ndiwa, watoto wake watatu na mhudumu wa bodaboada.

Kamanda wa Polisi wa Narok Reuben Lotiata alithibitisha kuwa mhudumu huyo wa bodaboda alikiri kusafirisha askari hao hadi bomani kwa Bw Ndiwa.

Polisi wanaendelea kumsaka Bw Ndiwa kuhusiana na mauaji hayo ya afisa wa cheo cha Inspekta Mkuu Patrick Kuya na mwenzake wa cheo cha sajini Daniel Nairimo katika kijiji cha Tepesonik, Trans Mara Magharibi.