Watanzania wawili kizimbani kwa shtaka la kuiba chupi

Watanzania wawili kizimbani kwa shtaka la kuiba chupi

Na Richard Munguti

RAIA wawili kutoka Tanzania wameshtakiwa kuiba chupi za wanawake za thamani ya Sh43,000.

Koduruni Laano almaarufu Masai na Patrick Kumongishu almaarufu Petrol walishtakiwa mbele ya hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bw David Ndungi.

Walikanusha shtaka la kuiba chupi hizo walipokuwa wakilinda bohari katika eneo la Koja Mosque Nairobi.Masai na Petrol walikataa kata kata kwamba waliiba chupi hizo mali ya mfanyabiashara Bi Jane Kamiru.

Raia hao wa kigeni walikana kuiba chupi hizo dazeni 22 mali ya Bi Kamiru na wakaomba waachiliwe kwa dhamana.Kiongozi wa mashtaka Bw Abel Omariba hakupinga dhamana ya mabawabu hao.

Aliomba korti iwaachilie kwa dhamana akisema jambo hilo litakuza ujirani Mwema kwa vile haki za washukiwa hao wa uhalifu zimezingatiwa.

Washtakiwa hao waliamriwa kulipa dhamana ya pesa tasilimu Sh10,000 kila mmoja pesa za Kenya.

 

You can share this post!

Kilio huku familia 800 zikibomolewa makazi

Watu 18,000 waokolewa kwa meno ya Taliban