Habari Mseto

Watatu wafariki kwenye ajali Bomet

November 17th, 2020 1 min read

NA VITALIS KIMUTAI NA FAUSTINE NGILA

Watu watatu wamefariki papo kwa hapo kwenye ajali ya barabara iliyotokea Jumanne iliyohusisha matatu na gari lililokuwa linaelekea kwenye barabara ya Bomet-Sotik.

Abiria tisa waliopata majeraha walipeekwa kwenye hospitali ya Tenwek kwa matibabu.

Kamanda wapolisi wa Bomet ya kati Musa Omari alisema kwamba tukio hilo lilifanyika saa tisa mchana.

“Matatu hiyo ilikuwa na abiria tis ana dereva ambaye alitoroka baada ya tukio hilo,”alisema Bw Omari.

Dereva huyo wa matatu alisemekana kuwa alikuwa akihepa kugoga mti wakati ajali hiyo ilitokea.

Mtatu hiyo iligogana kichwa kwa kichwa na gari hilo ndogo huku ikisabaishwa mguu wa gari kulipuka kabala ya kubingira mara kadhaaa na kuingia kwa shimo.

Abiria walirushwakutoka kwa viti hiyo ikisababisha majeraha na vifo,huku bidhaa zao zikitawanyiwa kwenye eneo la tukio.

Matatu inayomilikiwa na kampuni ya Egesa ilikuwa inasafiri kutoka Kisii ikielkea Nirobi wakati gari ambayo nambari yake ya usajili ijulikani ilikuwa ilielekea Kaplonga ziligongana.

Kati ya wale waliolazwa hspitalini ni dereva wa gari hilo ndogo. Miili ya waliofariki kwenye ajali hiyo ilipeelekwa kwenye hospitali ya rufaa ya Longisa .