Habari Mseto

Watatu wapigwa na radi wakichunga ng’ombe

March 3rd, 2024 1 min read

NA ERIC MATARA

WATU watatu wamelazwa katika hospitali mbalimbali za Narok na Bomet, baada ya kupigwa na radi walipokuwa wakichunga ng’ombe.

Wanaume hao watatu walipigwa na radi katika kijiji cha Kileleshwa huko Narok Kusini, Ijumaa, Machi 1, 2024.

Mmoja wa waathiriwa anaendelea kupata nafuu katika hospitali ya Longisa, Kaunti ya Bomet huku wengine wawili wakilazwa katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Narok ambapo wanapokea matibabu.

“Wanaume hao watatu walikuwa wakichunga ng’ombe katika shamba la Bw Jonathan Letina, radi ilipopiga. Walikimbizwa katika hospitali ndogo ya Ololulunga, kabla ya kuhamishwa hadi hospital zingine, ambapo wanapokea matibabu,” alifichua Naibu Kamishna wa Kaunti ya Narok Kusini Felix Kisalu.