Habari Mseto

Watatu watekwa nyara na Al Shabaab

October 4th, 2020 1 min read

NA MANASE OTSIALO

Watu watatu walitekwa nyara na wanamgambo wa Al Shabaab Kaunti ya Mandera Jumatano jioni.

Akithibitisha tukio hilo lililotokea saa kumi unusu jioni, mkuu wa uchunguzi wa maswala ya uhalifu Benedict Kigen alisema kwamba waathiriwa hao walikuwa mafundi waliokuwa wakieleka kazini mjini Lafey.

“Tukio hilo lilitokea kilomita 28 kutoka mji wa Lafey wakati gari la abiria lilipovamiva na watu wanaokisiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabaab  na waliokuwa waamejihami,” alisema Bw Kigen.

Alisema kwamba watatu hao walikuwa wageni Mandera.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA