Habari Mseto

Wateja wa KCB M-PESA kulazimika kulipia zaidi

August 3rd, 2019 1 min read

Na GEOFFREY ANENE

WATUMIAJI wa huduma ya mkopo ya KCB MPESA watalazimika kulipia zaidi.

Hii ni baada ya watoaji wa huduma hiyo kampuni za KCB Bank na Safaricom kutangaza kuongeza riba hiyo kutoka asilimia 4.08 hadi 7.5.

“Utaanza kulipia mkopo wako ujao wa KCB MPESA asilimia 7.5,” ilitangaza Agosti 2, 2019, kabla ya kuongeza “utahitajika kulipa mkopo wako ndani ya mwezi mmoja.”

Riba mpya ya KCB M-PESA inaenda sambamba na ile ya huduma nyingine inayotolewa na kampuni ya mawasiliano ya Safaricom na benki ya Commercial Bank of Africa.

KCB M-PESA ni mojawapo ya huduma za kutoa mikopo nchini ya riba ya chini.