Habari Mseto

Watisha kuroga yeyote atakayejaribu kuzuia tohara

August 26th, 2020 1 min read

Dennis Lubanga na Brian Ojamaa

Magharibi mwa Kenya sherehe za kutairi ni hafla muhimu ya kutoka utotoni hadi utu uzima ambayo imekuwa ikishereekewa kwa muda wa miaka mingi.

Hata wakati wa corona, hakuna jambo lolote linaloweza kuzuia sherehe hizo kulingana na wakazi.

Kulingana na Wabukusu wanaoishi kaunti za Bungoma, Kakamega, Transnzoia sherehe hizi hufayika kila mwezi wa nane, na mwaka huu mambo ni tofauti kwani janga la corona linaonekana kutatiza shughuli hio.

Kulingana na matatizo yaliyoletwa na virusi vya corona Wizara ya Afya imeweka mikakati hili kupunguza kusambaa kwa virusi vya corona huku watu wakilazimika kuacha shughuli zingine.

Lakini wazee wa Bukusu waliamua kwenda  kinyume na mikakati ya serikali na kuendeleza shughuli hiyo ya tohara.

Kuanzia mwezi Julai Wabukusu walipata usaidizi kutoka kwa majirani wao Tachoni na Batura na kuahidi kuroga mtu yeyote ambaye atajaribu kuwazuia kuendesha shughuli hiyo.

Wazee kutoka jamii hizo tatu walichaguliwa kuendesha shughuli hiyo huku wakizingatia mikakati ya Wizara ya Afya. Kwanza walifanya ibada ya kusafisha visu ambavyo vitatumika kwenye shughuli hiyo ya ukeketaji inayojulikana kama’khubita kimibano’.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA