Kimataifa

Watoto 22 waangamia kwa mavamizi ya angani Saudia

August 28th, 2018 1 min read

MASHIRIKA NA PETER MBURU

Umoja wa Mataifa (UN) Ijumaa ulitangaza kuwa mavamizi ya angani ya Saudi Arabia yaliua angalau watoto 22 na wanawake wanne nchini Yemen wakati wapiganaji wa taifa la awali walikuwa wakitoroka vitani.

Hilo, kulingana na UN ni vamizi la pili ambalo limeondoa maisha ya raia wengi wa Yemen mara moja katika kipindi cha wiki mbili.

Afisa mkuu wa UN nchini humo Mark Lowcock aliwekelea mzigo wa lawama kwa wapiganaji wa Saudi ambao wamekuwa wakivamiana na wanamgambo wa Yemen, kwa mavamizi hayo ya Alhamisi, karibu na ufuo wa Al Hudaydah, eneo la ziwa la shamu. Alisema vamizi jingine la hewani liliua watoto wanne.

Habari hizo zilizochapishwa kupitia wavuti wa ofisi ya Bw Lowcock zilikuja walkati wapiganaji wa Saudi walikuwa wakilimbikiziana lawama na wanamgambo wa Yemen kwa mavamizi hayo.

Sasa raia huko wanaishi kwa hatari, katika eneo ambalo limekuwa na vita kwa miaka mitatu sasa, UN ikitaja vita hivyo kuwa janga kuu zaidi ambalo limewahi kusababishwa na binadamu.

Pande zote mbili zimekuwa zikilaumiana kuhusu mathara yanayowaangukia raia wakati wa vita, haswa katika mavamizi ya hewani.

Lakini vikundi vya kutetea haki za binadamu na watetezi wa amani wamelaumu Marekani kwa kusambazia Saudi silaha, ripoti za ujasusi na ndege za vita, na kuisaidia kutekeleza mavamizi.

Japo pande zote mbili zimeshikilia kuwa zimekuwa zikifanya mavamizi ya kulenga vikosi hasimu vya kivita, Agosti 9 shambulizi lililotolewa na wapiganaji wa Saudi lilipata basi la shule eneo la Kaskazini mwa Yemen na kuua makumi ya raia, wakiwemo watoto.

Jumatatu, Rais Donald Trump wa Marekani alitia sahihi mswada ambao utawasilishwa mbele ya Saudi Arabia na Umoja wa Mataifa ya Kiarabu (UAE), zikisema kuwa zinafanya juhudi kuzuia vifo vya raia.