Habari Mseto

Watoto 5 wapatikana wameuawa

September 5th, 2020 1 min read

Na AFP

Watoto watano wamepatikana wakiwa wamefariki katika ghorofa moja Ujerumani. Kulingana na ripoti ya wanahabari, watoto hao waliuawa na mama yao ambaye alijaribu kujitia kitanzi baadaye.

Watoto hao walipatikana kwenye ghorofa ya kibinafsi mjini Solingen walisema polisi bila kutoa habarii zaidi.

Watoto hao walikuwa wa miaka mmoja, miwili, mitatu, sita na nane kulingana na ripoti ya gazeti ya Bild Daily.

Mamayao baadaye alijirusha mbele ya gari moshi lakini kwa bahati nzuri akahepa kifo lakini akapata majeraha mabaya ilisema ripoti hio. Aliokolewa na akapelekwa hospitali.

Nyanya ya Watoto hao ndiye aliyeita polisi na kuripoti kwamba mwanawe wa miaka 27 alikuwa ameua Watoto wake watano na kutoroka  na mtoto mmoja akiwa na nia ya kujiua.

Kijana wa miaka 11 wa mama huyo alipatikana akiwa salama ,ilisema ripoti hio.Uchunguzi bado unaendelea.

Tafsiri na Faustine Ngila