Watoto 88 wazaliwa Krismasi Eldoret

Watoto 88 wazaliwa Krismasi Eldoret

NA TITUS OMINDE

WANAWAKE 88 katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Moi MTRH mjini Eldoret walisherehekea Krismasi kwa kujifungulia katika kituo hicho wakati wa mkesha wa Krismasi na siku ya Krismasi.

Akina mama hao wenye furaha walisherehekea maisha mapya yaliyoletwa ulimwenguni katika kituo hicho kwa kuishukuru serikali kwa huduma za kujifungua bila malipo katika hospitali za umma has kitengo cha Mama na Mtoto cha MTRH Riley.

‘Nina furaha kubarikiwa na mtoto wa kiume wakati wa sherehe hii ya Krismasi. Nitamwita Emmanuel kunikumbusha kuzaliwa kwa Yesu Kristo,”alisema Sharon Rono, mmoja wa wanawake waliojifungua katika kituo hicho.

Wanawake hao walipongeza usimamizi wa hospitali hiyo kwa kuhakikisha viwango vya juu vya usafi katika kituo hicho ambacho ni hospitali ya pili kwa ukubwa ya rufaa nchini.

Akithibitisha kujifungua kwa akina mama hao Mkurugenzi Mtendaji wa MTRH Dkt Wilson Arausa alisema watoto wote 88 pamoja na mama zao walikuwa na afya njema baada ya kujifungua.

Dkt Aruasa alisema ni jambo la kufurahisha kutambua kwamba jumla ya watoto wachanga ambapo 44 kati yao walikuwa wavulana na wengine 44 walikuwa wasichana walizaliwa vyema wakati huu wa sherehe.

Alisema watoto wachanga 38 walizaliwa kati ya Desemba 25 na 26 wakati 50 kati yao walitolewa kati ya Desemba 24 na 25.

“Kama hospitali tunafurahi vivyo hivyo kupata mtoto huyu mchanga 88 wakati tunasherehekea Krismasi na Mwaka Mpya. Tunawatakia heri siku zote za maisha yao,”akasema Dkt Aruasa.

Wengi wa akina mama ambao walizaa siku ya Krismasi waliita watoto wao wa kiume Emmanuel ambayo inamaanisha ‘Mungu pamoja nasi.

Dk Aruasa alitoa changamoto kwa wanawake wengine kukubali wito wa serikali wa kujifungua watoto wao katika hospitali ili kuhakikisha kujifungua salama.

“Tuna kituo kizuri cha kujifungulia hapa, ninawahimiza akina mama wajawazito kukumbatia utamaduni wa kutembelea kliniki ya wajawazito na zaidi kuhakikisha kuwa wanajifungulia watoto wao hospitalini ili kujifungua salama kwa kufurahia sera ya serikali ya huduma za kujifungua bilamalipo, ” alisema Dkt Aruasa

You can share this post!

Wakazi wa Nairobi walia Krismasi imekuwa ‘kavu’

Ujanja wa Uhuru na Raila kuzima sauti zinazokosoa BBI