Watu 10,000 pekee kuhudhuria sherehe za Mashujaa Kirinyaga

Watu 10,000 pekee kuhudhuria sherehe za Mashujaa Kirinyaga

Na GEORGE MUNENE

WATU 10,000 pekee ndio wanaotarajiwa kuhudhuria sherehe za Mashujaa ambazo zitafanyika Oktoba 20 katika uga wa Wang’uru, Kaunti ya Kirinyaga na zitakazoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta.

Katibu katika Wizara ya Usalama wa Ndani Dkt Karanja Kibicho alisema ujenzi wa uga huo uliogharimu serikali mabilioni ya fedha, unatarajiwa kukamilika Oktoba 5 na baada ya hilo, uwanja huo utakuwa tayari kwa sherehe hizo.

Akizungumza katika mji wa Ngurubani baada ya kukagua ujenzi huo unaoendelea, Dkt Kibicho alisema idadi ya watakaohudhuria sherehe hizo ni watu 10,000 pekee kwa kuwa maambukizi ya corona bado yapo juu.

“Visa vya maambukizi vikiendelea kupanda, basi watu wachache tu wataruhusiwa kuhudhuria sherehe hizo,” akasema Dkt Kibicho.

You can share this post!

Afueni kwa wakazi wa Gatuanyaga barabara ikianza kujengwa

Chama cha Kingi chaanza kuvutia wanachama