Habari Mseto

Watu 11 zaidi waangamizwa na corona

October 12th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Wizara ya Afya imetangaza Jumatau kwamba watu 11 walifariki kutokana na virusi vya corona huku idadi kamili ya vifo ikifikia 777.

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe aliripoti visa vingine vipya 73 kutoka 388 vilivyoripotiwa Jumapili huku idadi ya maambukizi ikifikia 41,619.

Aliema kwamba maambuki hayo mapya yalipatikna baada ya sampuli 2,001 kupimwa idadi ya watu walipimwa virusi vya corona tangu corona iingie Kenya ni 593,199.

Waziri pia alisema  kwamba watu wengine 97 walipata nafuu kutokana na virusi hivyo huku 66 wakiruhiwa kwenda nyumbani huku idadi ya waliopona virusi vya corona ikifikia 31,097.

Kati ya wagonjwa hao ni Wakenya 46, wakiwa wanaume na 27. Mgonjwa mchanga zaidi ana miaka 17 huku mzee zaidi akiwa mika 77.

Nairobi ilikuwa na idadi ya 34, Kilifi 18, Mombasa 11, Busia 4, Taifa Taveta wawili na Kirinyanga, Meru na Uasin Gichu mmoja.