Habari Mseto

Watu 167 wapatikana na corona

June 7th, 2020 1 min read

NA BERNADINE MUTANU

Idadi ya wagojwa wa virusi vya corona imefikia 2,767 baada ya watu wengine 167 kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo kutokana na sampuli 2,833 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita.

Akitoa hotuba yake ya kila siku Waziri wa Afya Mutahi Kagwe alisema kwamba kati ya hao 167, 125 ni wanaumme na 42 wanawake.

Watu wengine 46 waliruhusiwa kwenda nyumbani huku idadi ya waliopona virusi vya corona imefikia 752.

Mtu mwingine mmoja amefariki kutokana na virusi vya corona huku idadi ya waliofariki kutokana na virusi hivo ikifika watu 84. Nairobi inaongoza kwa maambukizi ikiwa na idadi 1,235.

Alisema kwamba msimamo wa serikali wa kufungua maeneo ya burudani na uuzaji wa pombe ni uleule.

Waziri Kagwe aliwashukuru wazee wa nyumba kumi wanaoripoti visa vya corona vikitokezea vijijini.

“Kufunguliwa kwa maeneo ya burudani na uzaji wa pombe ni marufuku na watakaokiuka masharti haya leseni zao zitachukuliwa,” alisema Bw Kagwe.