Kimataifa

Watu 36 kunyongwa kwa kuvamia makanisa ya Coptic

April 11th, 2018 1 min read

Na MASHIRIKA

CAIRO, MISRI

MAHAKAMA ya jeshi imewahukumu watu 36 kunyongwa kwa kuhusika katika mashambulizji dhidi ya makanisa ya Kikristo ya Coptic nchini Misri, mawakili wao wamesema.

Kulingana na mawakili hao, watu 48 wamekuwa wakifuatiliwa kuhusu uvamizi huo katika miji ya Cairo, Tanta na Alexandria kati ya mwaka 2016 na 2017.

Uvamizi huo ambao kundi la kigaidi la Islamic State (IS) lilikiri kutekeleza, ulisasabisha vifo vya watu 80.

Wakristo wa makanisa hayo, ambao ni asilimia 10 ya raia milioni 96 wa Misri, wamekuwa wakilengwa sana na kundi la kigaidi la IS.

Maoni kuhusu ya viongozi wakuu wa dini nchini Misri huibuka kila wakati hukumu ya kifo hutolewa na mahakama, lakini hayatambuliwi kisheria.