Watu 4 wafariki katika ajali ya ndege ya mizigo ya Urusi

Watu 4 wafariki katika ajali ya ndege ya mizigo ya Urusi

NA AFP

MOSCOW, URUSI

WATU wanne wamefariki Ijumaa na wengine watano wakajeruhiwa ndege ya mizigo ya Urusi ilipoanguka katika mji wa Ryazan, kusini mashariki mwa Moscow, watawala wamesema.

Ajali hiyo ilitokea ndege ilipokuwa ikijaribu kutua baada ya kukumbwa na hitilafu.

Ndege hiyo ambayo haikuwa imebeba mizigo iliharibika baada ya kugonga ardhi kwa kishindo, wizara ya ulinzi ikasema kwenye taarifa.

“Kulingana na habari za awali, watu wanne walikufa kutokana na ajali ya ndege katika eneo la Mikhailovsky mjini Ryazan,” shirika la kukabiliana na majanga katika serikali ya jimbo, limesema katika taarifa.

Wizara ya Ulinzi, kupitia shirika la habari la TASS, imesema kuwa wahudumu wa ndege hiyo waliojeruhiwa walikimbizwa hospitalini.

TAFSIRI NA: CHARLES WASONGA

  • Tags

You can share this post!

CECIL ODONGO: Viongozi wa Mulembe hawafai kumlaumu Raila...

WANDERI KAMAU: Mataifa ya Afrika yaungane kupata ufanisi wa...

T L