Kimataifa

Watu 45 waaga dunia nchini Afrika Kusini katika ajali barabarani

March 29th, 2024 1 min read

NA MASHIRIKA

WATERBERG, AFRIKA KUSINI

WATU 45 wameaga dunia, na mmoja akajeruhiwa, katika ajali iliyohusisha basi moja katika mkoa wa kaskazini wa Limpopo, Afrika Kusini.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Wizara ya Uchukuzi dereva wa basi hilo alipoteza mwelekeo na kugonga nguzo ya barabara katika daraja moja karibu na mji wa Waterberg.

Basi hilo lilianguka na kushika moto katika ajali hiyo iliyotokea Alhamisi jioni.

Lilikuwa likiwasafirisha watu kutoka taifa jirani la Botswana kwa sherehe za Pasaka katika mji wa Moria mkoani Limpopo.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alituma risala zake za rambirambi na pole kwa taifa la Botswana na kuahidi kutoa msaada kwa familia za walioangamia.