Watu 5 waangamia kwenye ajali

Watu 5 waangamia kwenye ajali

NA MWANDISHI WETU

Watu watano waliangamia kwenye ajali hapo Jumamosi katika barabara kuu ya Nakuru kuelekea Kericho.

Ajali hiyo iliyohusisha lori na magari mengine matano ilitokea katika kaunti ya Kericho.

Musa Kongoli, OCPD wa Londiani, alisema kuwa dereva wa lori hilo alikuwa akielekea Kericho akitoka Nakuru alikpopoteza mwelekeo na akagongana na matatu iliyokuwa ikielekea Nakuru ikitoka Kericho.

Magari mengine manne yalihusika katika ajali hiyo iliyosababisha kifo cha wanawake wawili na wanaume watatu.

“Inahuzunisha sana kupoteza watu watano kwa ajali hii. Walioumia walikuwa kwenye matatu. Dereva wa lori alipata majeraha na akakimbizwa hospitalini,” alisema Bw Kongoli.

Alisema kuwa wengine kumi na wawili wanatibiwa hospitalini.

Tafsiri: Faustine Ngila

You can share this post!

NASAHA ZA RAMADHAN: Tudumishe heshima ya juu...

Chelsea yakubali ombi la Kante kutorejea kambini kwa...

adminleo