Leicester inafaa kujilaumu kubanduliwa Ligi ya Uropa

Leicester inafaa kujilaumu kubanduliwa Ligi ya Uropa

LEICESTER, Uingereza

KOCHA Brendan Rodgers amekiri kuwa Leicester City haifai kulaumu yeyote isipokuwa wao wenyewe baada ya kubanduliwa kwenye Ligi ya Uropa mnamo Alhamisi.

Mechi ya nipe-nikupe dhidi ya wenyeji Napoli ilishuhudia timu hizo zikienda mapumzikoni 2-2 ugani Diego Armando Maradona mjini Naples.Napoli ya kocha Luciano Spalletti iliongoza 2-0 kupitia mabao ya Adam Ounas na Eljif Elmas katika dakika 24 za kwanza ambazo makocha rasmi wa Leicester hawakuwa wamefika uwanjani baada ya polisi kuwapotosha njia.

Hata hivyo, ‘Foxes’ walijibu kupitia kwa Jonny Evans na Kiernan Dewsbury-Hall katika dakika tisa zilizofuata kabla ya Elmas kufungia Napoli la tatu dakika ya 53. Licha ya vijana wa Rodgers kupata nafasi nyingi nzuri za kusawazisha tena, hawakufua dafu.

Leicester iliongoza Kundi C kabla ya mchuano huo. Hata hivyo, kipenga cha mwisho kilipolia ilikuwa imetupwa hadi nafasi ya tatu. Imeingia mashindano ya daraja ya tatu ya Europa Conference League baada ya Spartak Moscow kushinda kundi hilo kwa kuzima Legia Warsaw 1-0.

“Tunasikitika, lakini si vyema kujipata katika hali unahitaji kufunga mabao matatu ama manne kuzoa ushindi. Lazima ufanye kazi yako vyema kufuzu,” alisema kabla ya kushangaza kuwa hana habari kuhusu Europa League Conference.

Washindi wa makundi yote manane ya Ligi ya Uropa waliingia raundi ya 16-bora moja kwa moja. Nambari mbili kutoka kila kundi watapambana na timu nane zilizokamilisha Klabu Bingwa Ulaya katika nafasi ya tatu kupata tiketi ya awamu hiyo.

 

 

 

You can share this post!

MESPT inavyojituma kupiga jeki sekta ya kilimo nchini na...

Mbunge Hassan aomba baraza la kiswahili kubuniwa nchini

abdul9597129561