Watu 6 kati ya 10 Uganda wahofia huenda uchaguzi ukalitumbukiza taifa kwenye ghasia

Watu 6 kati ya 10 Uganda wahofia huenda uchaguzi ukalitumbukiza taifa kwenye ghasia

Na FRANKLIN DRAKU

KAMPALA, Uganda

SITA kati ya raia 10 wa Uganda wameingiwa na hofu kufuatia ghasia zinazoshuhudiwa nchini humo wakati huu wa kampeni za kuelekea uchaguzi, kulingana na kauli za wapigakura katika utafiti ulioendeshwa na shirika moja la asili ya Amerika.

Shirika hilo, The International Foundation for Electoral Systems (IFES) lenye makao yake mjini Arlington, jimboni Virginia, linasema vijana na maafisa wa vyama vya kisiasa ndio wanakabiliwa na hatari zaidi ya kuathiriwa na ghasia hizo.

Wengine wanaokabiliwa na hatari ya kuathiriwa na ghasia hizo za uchaguzi nchini Uganda ni wanaharakati wa kutetea haki, wanawake, wanahabari, watu wanaoishi na ulemavu na wanachama wa makundi ya wachache.

IFES inafadhiliwa na serikali ya Amerika na mashirika mengine katika mataifa yaliyoendelea. Hushirikiana na makundi ya mashirika ya kijamii, asasi za umma na sekta ya kibinafsi kuendeleza utawala wa kidemokrasia kwa manufaa ya wote, kulingana na habari katika wavuti wake.

Mwezi mmoja baada ya kuanza kwa kampeni za urais, ulioratibiwa kufanyika mnamo Januari 14, 2021, kumeshuhudiwa mapigano kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa wagombeaji wa upinzani.

Ghasia hizo zilishamiri mnamo Novemba 18 na Novemba 19 ambapo polisi walisema watu 54 waliuawa wakati wa makabiliano kati yao na wafuasi wa mgombeaji wa urais kwa tiketi ya chama cha National Unity Platform, Robert Kyagulanyi, ambao walikuwa wakipinga kukamatwa kwake.

  • Tags

You can share this post!

Sonko amejihami vilivyo kuokoa kazi yake isimtoke

Watu 18 wafa kwenye mgodi China